Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 10: Kwenda mgahawani > Lesson 6:

    

VYAKULA VYA MGAHAWANI

Kwanza karibuni mgahawa wa New Happy. Katika mgawaha huu, kama migahawa mingine mingi katika mji wowote Tanzania, unaweza kupata vyakula na vinywaji mbalimbali. Vyakula vyote vinapikwa jikoni katika mgahawa huu. Twende tuwatembelea wapishi wa mgahawa huu. Kuna vyakula vingi. Unaweza kuona vyakula kama samaki wa kukaanga, viazi vya kukaanga au chipsi, kuku wa kukaanga, ugali, mchicha, sosi ya nyanya, matoke ya nyama, wali, saladi ya kabeji, na sosi ya kuku.

© African Studies Institute, University of Georgia.