Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 9: Usafiri wa majini > Lesson 6:

    

KWENDA VISIWA VYA GEDE NA UNGUJA

Mji wa Zanzibar ni mji mdogo sana. Si lazima kuwa na motokaa. Watu wengi wanatambea kwenda ofisini, kazini, sokoni, na madukani. Wachache wanatumia baisikeli.

Unaweza kwenda Unguja kwa ndege au meli ndogo. Waswahili wa Unguja husema boti badala ya meli. Kwa ndege, kutoka Tanzania bara ni dakika ishirini hivi. Kwa boti ni saa moja na nusu.

Sasa tutaondoka Malindi na kutembelea mji mdogo wa Gede. Zamani Gede ndimo mlimokuwa makao makuu ya sehemu hizi. Sasa shughuli zote za serikali hufanyika mjini Malindi. Wasafiri wanaokwenda Gede hutumia dau zenye tanga zinazosukumwa na upepo. Mji wa Gede ni mji maarufu kwa historia yake iliyohifadhiwa katika magofu ya nyumba zake za zamani, na pia jumba la makumbusho ambalo hutunzwa sana na serikali ya Kenya. Tujiunge na wasafiri hawa kwenda Gede.

© African Studies Institute, University of Georgia